Magwiji wa Kiswahili, Miigo ya KCSE ni kitabu kimojawapo katika msururu wa Achievers KCSE Revision, ambacho kimeandikwa kwa madhumuni ya kuwasaidia wanafunzi kujiandaa katika mtihani wa KCSE. Kitabu hiki kinampa mtahiniwa na mwalimu taswira halisi ya karatasi za KCSE. Kila kitabu katika msururu huu kina miigo kumi ya KCSE ambayo inafuata mtindo mpya. Aidha, mwongozo wa kusahihisha karatasi zote umetolewa.
Magwiji wa Kiswahili, Miigo ya KCSE ni kitabu ambacho kina muhtasari wa karatasi zote tatu za Kiswahili ambazo ni insha; ufahamu, muhtasari na matumizi ya lugha pamoja na fasihi. Vipengele muhimu vya kumwezesha mwanafunzi kufanya vizuri katika mtihani wa KCSE vimeelezwa kwa ufupi na ukamilifu.
Aidha, kitabu kina miigo ya KCSE ambapo maswali kutoka katika vitabu vipya vya fasihi yamezingatiwa.
Mwanafunzi yeyote anayetumia kitabu hiki ana uhakika wa kukwangura alama za juu katika mtihani wake.
Vipengele muhimu vya kitabu hiki: :
- uchanganuzi wa maswali ya KCSE yaliyowahi kutungwa pamoja na yale yanayotarajiwa;
- vidokezo muhimu kuhusu ni kwa nini wanafunzi hupoteza alama hata kama jawabu lililotolewa ni sahihi;
- utangulizi murwa wenye vidokezi muhimu vya kumfaa mtahiniwa;
- muhtasari wa karatasi zote tatu ambazo ni insha, matumizi ya lugha na fasihi;
- maswali anuwai kutoka kwenye vitabu vipya vya fasihi na mwongozo wa kusahihisha kwa maswali hayo;
- sehemu ya mwongozo wa kusahihisha yenye kuonesha hatua kwa hatua namna anavyotuzwa.
Waandishi wa kazi hii babukubwa, Simon Ngige na Justus Kyalo Muusya ni walimu wenye tajriba pana ya ufundishaji wa Kiswahili katika shule mbalimbali nchini Kenya. Aidha, ni watahini wa KCSE wenye kuaminika.