Unaweza ukawa gwiji mkuu!
Vitaby vya Miigo ya KCSE ni msururu mpya uliotungwa kispesheli kukufanya wewe kuwa gwiji. Kila kitabu katika msururu huu kimeandikwa na walimu na watahini wenye tajriba pevu. Wameitalii silabasi ya shule za msingi na kutunga maswali yenye kina kikuu huku wakizingatia kwa karibu sana mtindo unaotumiwa na mtihani wa KCPE. Kwa mtahiniwa, vitabu hivi ndivyo njia ya hakika ya kuelekea kwenye upeo wa ufanisi katika mtihani wa KCPE. Kwa mwalimu na mtahini, vitabu hivi ndivyo miongozo ya hakiki ya mitihani.
Magwiji wa Kiswahili, Miigo ya KCPE ni kitabu cha aina yake cha udurusu ambacho:
- kina miigo 20 ya mtihani wa KCPE ambayo inafuata mtindo wa utahini pamoja na mfumo wa uteuzi wa maswali ya KCPE.
- kina vidokezo muhimu vya namna ya kufanikiwa katika mtihani wa Kiswahili wa KCPE.
- kina majibu kwa maswali yote.
- kimeandikwa kwa mtindo sahili na unaovutia sana ambao unarahisisha matumizi.
- kina maagizo ambayo hutolewa na Baraza la Mitihani la Kenya kwa kila karatasi ya mtihani wa KCPE.
Vitabu Vingine katika msururu huu:
- Achievers Mathematics Model KCPE Examination Papers.
- Achievers English Model KCPE Examination Papers.
- Achievers Science Model KCPE Examination Papers.
- Achievers Social Studies & Christian Religious Education Model KCPE Examination Papers.
Msururu wa Vitabu vya Miigo ya KCPE ndiyo ngazi ya hakika ya kuafikia ndoto yako unayoienzi!