,

Kiswahili Angaza Gredi 3

KSh225 "Does not include Tax"

MwandishiShabaan Otieno & Mziwanda Banda
Mchapishaji: East African Educational Publishers
Mwaka: First published 2018
ISBN: 978-9966-56-286-9


  1. Select Book Type in the drop-down button below (Print Book or e-book).
  2. Click on ADD TO CART.
SKU: N/A Categories: , Tags: ,

Kitabu cha Mwanafunzi

Kiswahili Angaza ni kozi iliyosukwa na kuwambwa kwa makini na kwa kina kirefu. Imetimiza kwa ukomo wa ukamilifu mahitaji ya mtalaa mpya wenye kuzingatia umilisi, yaani, Competency-Based Curriculum, 2018. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo unaomwegemea mwanafunzi zaidi na kumfanya mwalimu awe mwelekezi tu wala si mtoaji wa elimu. Kitabu hiki kinazingatia mambo matano muhimu:

1. Kusoma ni kutagusana; wanafunzi wanafanya Shughuli mbalimbali wakiwa peke yao, wawili wawili au katika makundi;
2. Wanafunzi wanaanza kila somo kwa kuelezea picha au hali ama matukio wanayoyafamu huku wakijadiliana;
3. Wanafunzi wanashiriki katika stadi nyingi za kufikiria  kama vile kuchanganua, kutambua, kubainisha, kujenga na kuhakiki;
4. Lugha iliyotumika ni nyepesi mno na isiyokuwa na maneno magumumagumu na misamiati ya kubabaisha;
5. Mwanafunzi na mwanafunzi mwenzake, pamoja na mwalimu, mzazi na hata jamii nzima wanashirikishwa ndani ya kitabu hiki.
Ili kuhakikisha kwamba mwanafunzi anashiriki katika utendaji wakati wa somo, Shughuli mbalimbali zinazopalilia na kushadidia umilisi wake zimezingatiwa. Shughuli hizo ni kama zifuatazo: Shughuli za Darasa; Shughuli za Kibinafsi; Shughuli za Makundi; Shughuli za Wawili wawili; Shughuli za Nyumbani; Shughuli za Nje ya darasa; Shughuli Mseto; Shughuli za Ziada na Shughuli za Utafiti.
Book Type

Print Book, e-book