Kitabu cha Mwalimu
Kiswahili Angaza, Mwongozo wa Mwalimu ni kitabu kilichosukwa na kuwambwa kwa makini na kwa kina kirefu. Kimetimiza kwa ukomo wa ukamilifu mahitaji ya mtalaa mpya wenye kuzingatia umilisi, yaani, Competency-Based Curriculum, 2018. Mwalimu ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa mtalaa mpya. Itakuwa vigumu kwa wanafunzi pekee kujiongoza katika mtalaa huu. Mwongozo huu hivyo basi unatoa mwelekeo ufaao kwa mwalimu na kumwongoza hatua kwa hatua katika ufundishaji. Kitabu hiki kinazingatia mambo saba muhimu:
- Utangulizi unaozungumzia kwa mapana na marefu mtalaa mpya unaomwegemea mwanafunzi, mbinu, nyenzo na asilia mbalimbali za kutumia katika ufundishaji pamoja na mambo mengine ainati;
- Kifano cha maazimio ya kazi pamoja na andao la somo kwa kutumia mtindo mpya uliopendekezwa na KICD;
- Ripoti ya maendeleo ya mwanafunzi inayofaa kujazwa mwishoni mwa kila mada kuu. Ripoti hii inafaa kujazwa na mwalimu pamoja na mzazi au mlezi;
- Utangulizi kwa kila somo. Kila utangulizi una jedwali linaloonyesha wiki ya somo, mada kuu, mada ndogo, nyenzo na idadi ya vipindi.
- Kabla ya somo lenyewe, mwalimu anaonyeshwa shabaha ya kila somo, umilisi wa msingi unaokuzwa, uhusiano na masuala mtambiko, shughuli za huduma za kijamii, uhusiano na maadili, uhusiano na masomo mengine na mapendekezo ya tathmini.
- Hatimaye, mwalimu anaonyeshwa hatua mbalimbali za kufundisha somo lake tangia kuingia darasani hadi mwisho wa somo.
- Mahitaji ya wanafunzi wenye uwezo mbalimbali aidha yameshughulikiwa.
- Lugha iliyotumika ni nyepesi mno na isiyokuwa na maneno magumumagumu na misamiati ya kubabaisha.