EAEP Kitabu cha Mazoezi, Gredi ya 4 ni kitabu kilichoandikwa kwa ubunifu ili kuimarisha maarifa ya mwanafunzi kupitia mazoezi. Mazoezi kwenye kitabu hiki yamewasilisha kikamilifu mahitaji ya Mtalaa wa Umilisi. Mazoezi haya yatamwezesha mwanafunzi kukuza stadi zinazohitajika, maadili na kukabiliana na masuala mtambuko. Kitabu hiki kimezingatia mambo muhimu katika ujifunzaji wa lugha:
- Mazoezi mbalimbali yanayopalilia na kushadidia umilisi wa mwanafunzi.
- Kimeangazia stadi zote za kujifunza lugha ambazo ni:
Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika. - Muhtasari unaoeleza yale yatakayoshughulikiwa kwa kila stadi ya ujifunzaji.
- โSasa ninajuaโ na โSasa ninawezaโ ambavyo ni vidokezo vya kujifunzia na kuimarisha umilisi baada ya mazoezi.
- Kimetumia lugha nyepesi iliyokomaa na inayoweza kueleweka na mwanafunzi kwa urahisi.
- Picha zilizotumika zimechorwa vizuri na kikamilifu. Kila mada imeanza kwa picha ambayo inasisimua hamu ya mwanafunzi ya kujifunza.
Waandishi wa kitabu hiki wana uzoefu mwingi na wamekiandika kitabu hiki kwa utaalamu mkuu. Ndio waandishi wa vitabu maarufu vya Kiswahili Angaza Gredi ya 1, 2, 3 na 4.