3. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali Maridhia alikuwa pale jukwaani akiwa miongoni mwa waalikwa mahususi katika shule ya upili ya wasichana ya Twapambazuka. Hii ilikuwa shule ya kipekee iliyokuwa imejengwa hivi majuzi kutokana na michango ya wafadhili na marafiki fulani wa chanda na pete wa Maridhia.
Maridhia alipokuwa pale jukwaani aliwatupia macho wanafunzi waliokuwa wamejaa pomoni pale ukumbini. Kisha akajisernea kimoyomoyo, 'Wanafunzi hawa wana bahati ya mtende. Wangejua kilichowapata wasichana wa enzi zetu, katu wasingezembea masomo. Wangejua hatua kubwa iliyopigwa na dada zao wangewaiga na kuzidi kufungua macho na kuikumbatia hamu ya kusoma zaidi. Sijui nitatumia lugha au mbinu gani leo kuwahamasisha!'
Rafikiye Maridhia, aliyekuwa mmoja wa wageni, alipomwona Maridhia kadidimia mawazoni alimgutusha. 'Hee! Maridhia, mbona hivyo? Unawazia nini?' Maridhia aliyaficha macbozi yaliyokuwa yanayaziba macho yake, machozi yaliyotokana na kumbukumbu ya yale aliyoyapitia hadi kufikia pale. Kisha akajutia purukushani na kumjibu, 'Hakuna jambo la maana la kuwazia sasa. Ya kale hayanuki. Sasa nataka nigange yajayo.' Wakaendelea kusikiliza hotuba hizi na zile za kusifu hatua mbalimbali zilizopigwa katika kuinua kiwango cha elimu cha wanawake pale pao Shimoni. Mara kwa mara Maridhia alisikia jina lake likitajwa na kumiminiwa sifa kemkem na shukrani tele.
Maridhia alizirudisha fikira zake nyuma tena, akakumbuka vile alivyosoma kwa shida licha ya kuwa wazazi wake hawakuwa wachochole. Alikumbuka vile wazazi hao walivyomnyima fursa ya kujiunga na shule ya upili kwa kufuata misimamo hasi ya wakazi wa Shimoni wa wakati huo. Hawa waliandama fikira kuwa kumsomesha msichana ni kupoteza mali bure. Wazazi wa Maridhia, kwa kuongozwa na tamaa, wakamuoza kwa babu mmoja mkwasi kupindukia. Ilibidi Maridhia akubali uamuzi huu shingo upande. Maridhia alikumbuka jinsi alivyoteseka katika ndoa hiyo. Alikumbuka vipigo vya kila mara, vicheko, vitisho na kuaibishwa hadharani na jamii, hasa ilipotokea kuwa amechelewa kuipata mbeleko . Mambo yalipomfika kooni akasema, 'Potelea mbali, liwe liwalo, hata wakisema mwacha mila ni mtumwa ni sawa. Maneno matupu hayavunji mifupa.' Baada ya kuwaza na kuwazua Maridhia alitafuta maarifa ya kujinasua, akamwendea Bi Salama na kumlilia shida. Bi Salama alimshauri ajiunge na kituo cha elimu ya watu wazima. Huko Maridhia alipewa mafunzo mengi. Alitia shime masomoni akiamini kuwa kisomo hakina umri wala mwisho, akasoma hadi chuo kikuu.
Baada ya kuhitimu chuoni alirudi kwao na kupata kazi ambayo ilimwezesha kuwakimu wazazi wake waliokuwa wazee. Aidha alianzisha miradi mbalimbal Shimoni. Mafanikio ya Maridhia yaliwasuta na kuwaaibisha kindanindani wale waliomdbulumu awali. Wengine walimsingizia hili na lile. Hata hivyo, hawangeweza kufanya lolote kuizima kiu ya Maridhia ya kujiendeleza. Maridhia aliwapuuza akisema kuwa asilani jua haliwezi kuzuiwa kwa ungo.
Miaka mitatu baada ya Maridhia kupata kazi walirudiana na mumewe. Mumewe alimwomba msamaha naye Maridhia akamsamehe. Aliwasamehe pia wote waliomtesa. Aliwaona
kuwa walioongozwa na itikadi zilizopitwa na wakati. Aliwaelimisha wanakijiji kuwa ni muhimu kumsomesha mwanamke pia. Wasibague. Mwanamke mmoja akielimishwa, huelimisha dunia. Maneno ya Maridhia yalimtoa nyoka pangoni, watu wakawasomesha wana wa jinsia zote, Shimoni ikaanza kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Shule zilijengwa, miundomsingi kama vile barabara ikaimarishwa na hospitali zilizokuwepo zikaboreshwa. Maji ya mabomba yalisambazwa vijijini, chombo kilichokuwa kinaelekea kuzama kikaokolewa.
Sifa za Maridhia zilivuma pembe zote za Shimoni na jamii jirani . Wazazi na walezi waliwapigia watoto wao mfano wa Maridhia ambaye aliweza kuzikosoa mila duni na akafaulu. Jambo hilo lilionekana kuwa mwiko hapo awali. Jarnii nzima ilifunguka macho; Maridhia akawa kielelezo, si kwa vijana wa kike tu, bali pia kwa vijana wa kiume, wazazi na jamii kwa jumla.
Maana ya: 'kuipata mbeleko', ni: