9. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo. Dunia haishi upya ingawa za zamani. Hii ina maana kuwa ulimwengu hauishi mambo mapya kila wakati. Hatupaswi kushangaa tunapoyaona mambo mapya ulimwenguni. Binadamu amepiga hatua kubwa sana kuyaleta mabadiliko. Teknolojia imechangia pakubwa katika kuyafanikisha mabadiliko hayo. Maendeleo haya ya kiteknolojia yameufanya kuwa kama kijiji kidogo.
Teknolojia hii imechangia pakubwa katika kuyarahisha maisha. Mawasiliano yamekuwa rahisi. Katika enzi za kisogoni, iwapo mtu alitaka kuufikisha ujumbe,alilazimika kuwatuma wajumbe. Aghalabu,makatikiro wangechelewa au kubadilisha ujumbe. Isitoshe, waliotuma barua, wangesubiri kikonzo; kwa muda mrefu. Mambo sasa yamekuwa mswaki. Kwa kutumia simu, unaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali kwa urahisi.
Hapo zamani yalikuwa mazoea kusikia kuwa faili zimepotea hasa kortini. Hayo sasa yamezikwa katika kaburi la sahau.Ukitaka kupata habari kuhusu mtu au jambo fulani, utabofya tu jina kwenye tarakilishi. Maelezo yote yatajianika kwenye kiwambo cha runinga. Kule kuhangaika kubukua matope ya faili na majadala kumeisha.
Hapo zamani hasa mwisho wa mwezi, watu wangepiga foleni ndefundefu kupata huduma mbalimbali. Siku hizi mambo ni tofauti. Huduma za maji, umeme, benki na hkadhalika hulipiwa kupitia kwenye simu. Huduma za pesa kam vile M-PESA zimefanya maisha kuwa mswaki. Unaweza kulipia huduma yoyote, wakati wowote ukiwa mahali popote. Raha iliyoje!
Mbali na hayo, masomo ya mitandaoni yameinua na kuimarisha elimu nchini. Mradi uwe na kompyuta iliyounganishwa kwenye mtandao, unaweza kuendeleza masomo. Si lazima uende shule wala darasani. Aidha, mtu husoma kwa raha zake wakati wowote anaotaka. Watu wengi wamepata diploma na shahada wakiwa nyumbani au hata ofisini. Hakuna kutoa visingizio kuwa huna wakati a kusoma, la hasha! Yeyote mwenye nia kusoma, anaweza kusoma bila udhia.
Teknolojia ndio njia. Hakuna kupoteza wakati tena . Wananchi wanapata fursa ya kufanya shughuli nyingine muhimu za ujenzi wa taifa. Kupitia kwa teknolojia unaweza kununua bidhaa au kuagiza huduma yeyote kupitia kwenye simu. Je, umeyasikia magari ya teksi yanayoitwa UBER? Ukitaka kwenda popote, unaiagiza kwa simu na kuilipia kwa simu.
Hati hivyo, hakuna bamvua lisilo na usubi. Licha ya manufaa yanayotokana na teknolojia, ina madhara pia. Awali ya yote, imezorotesha pakubwa maadili katiak jamii. Vijana wamepotoka maadamu wanayaiga kikasuku mabaya na maovu wanayoyaona mtandaoni.Mitindo ya kisasa ya mavazi ni ya aibu na ya kumtapisha hata nguruwe! Mazungumzo nayo hayana tafsida hata chembe yanakirihisha ajabu
Fauka ya hayo, vijana wamepevuka katika mambo yasiyolingana na umri wao. Wanayajua masuala ya mapenzi katiak umri usiofaa. Hili limechangia katika kujitosa katika bahari ya mapenzi wakiwa wachanga mno. waama, teknolojia imebwaga zani duniani.
Isitoshe, teknolojia imeeneza uzembe na uzohali miongoni mwa watu. Baadhi ya watu hutumia uda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii mathalan: Facebook, Twita, Whatsapp na instagramu. Ofisini badala ya kuchapa kazi, watu huzama mitandaoni. Hali ikiendelea hivi duniani itageuka kuwa ulimwegu wa wazembe.
Teknolojia ni kama upanga wenye makali pembe mbili. Ikitumiwa vibaya itatuhasiri na kutudhuru. Hata hivyo, ikitumiwa vyema na kwa tahadhari, itatunufahisha na kutufahidi pakubwa. Tuwe waangalifu la sivyo maarifa yetu ndiyo yatakayotuangamiza. Kumbuka, akili ya mtu ndiyo wazimu wake.
Mtazamo wa mwandishi kuhusu teknolojia ni kuwa?